Monday, 23 January 2017

Walter Nbaga mwenyewe


Mkuu wa wilaya ya Mbulu akemea Mila potofu katika jamii...

Wananchi wilayani mbulu wametakiwa kuacha mila potofu ya ukeketaji kwani zinaleta madhara kutokana na vitendo hivyo .
Hayo yamebainiswa na mkuu wa wilaya ya mbulu Bw. Chelestino Simbalimile Mofuga amesema vitendo hivyo vinafanyika kwa usiri na amewataka wananchi waache mila hizo potofu.

Kwa upande wao viongozi wa dini wamesema majukwaa ya ibada yana nafasi kubwa  kama yalivyo majukwaa mengine katika kupambana  na ukeketaji.


Mkuu wa wilaya ametoa rai kwa viongozi wa dini kukemea maovu ili jamii iweze  kubadilika. 
= = = = == = = 

Rais Erdogan afika Tanzania na Habari Njema, Mikataba 9 na wafanyabiashara zaidi ya Mia



Serikali za Tanzania na Uturuki zimesaini mikataba 9  ya ushirikiano wa kimaendeleo baada ya kuwasili kwa Rais wa Uturuki kwa ziara ya kikazi ya siku mbili nchini.

Akizungumza baada ya kutiliana saini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amesema, ujio wa Rais wa rais huyo  umejumuisha wafanyabiashara 150 na kwamba, mikataba iliyosainiwa itasaidia kukuza uchumi pamoja na mahusiano baina ya mataifa hayo mawili.

Rais Magufuli ameitaja baadhi ya mikataba iliyosainiwa kuwa ni ya sekta za afya, elimu, ulinzi, na  viwanda na kumwomba Rais Erdogan kuikopesha Tanzania kiasi cha fedha kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kisasa ya Standard Gauge yenye urefu wa zaidi ya kilometa 400

Rais Magufuli pia amesema Rais huyo amekubali kuongeza nafasi za wanafunzi wanaokwenda kusoma nchini Uturuki kutoka idadi ya wanafunzi 48 iliyopo imekubali kutoa mafunzo ya ulinzi kwa watanzania nchini Uturuki.


Hadi sasa kampuni 30 za Uturuki zimefanya uwekezaji nchini Tanzania wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 305.08.
 = = = = = = =