Serikali za
Tanzania na Uturuki zimesaini mikataba 9 ya ushirikiano wa kimaendeleo baada ya
kuwasili kwa Rais wa Uturuki kwa ziara ya kikazi ya siku mbili nchini.
Akizungumza baada ya kutiliana saini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amesema, ujio wa Rais wa rais huyo umejumuisha wafanyabiashara 150 na kwamba, mikataba iliyosainiwa itasaidia kukuza uchumi pamoja na mahusiano baina ya mataifa hayo mawili.
Rais Magufuli ameitaja baadhi ya mikataba iliyosainiwa kuwa ni ya sekta za afya, elimu, ulinzi, na viwanda na kumwomba Rais Erdogan kuikopesha Tanzania kiasi cha fedha kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kisasa ya Standard Gauge yenye urefu wa zaidi ya kilometa 400
Rais Magufuli pia amesema Rais huyo amekubali kuongeza nafasi za wanafunzi wanaokwenda kusoma nchini Uturuki kutoka idadi ya wanafunzi 48 iliyopo imekubali kutoa mafunzo ya ulinzi kwa watanzania nchini Uturuki.
Hadi sasa kampuni 30 za Uturuki zimefanya uwekezaji nchini Tanzania wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 305.08.
= = = = = = =
The best poker sites for Baccarat - Expert Analysis
ReplyDeleteLearn how to play at Baccarat with our extensive experience of live dealer games including poker, blackjack and roulette games from 온라인 바카라 게임 a variety of providers.